Migogoro
Thailand yatangaza amri ya kutokutoka nje
14 Desemba 2025
Matangazo
Hayo yanajiri ikiwa ni siku mbili tangu Rais wa Marekani Donald Trump aliposema viongozi wa nchi hizo wamekubali kusitisha mapigano. Viongozi wa Thailand hata hivyo wamesema hakuna makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa.
Mtafaruku wazidi maeneo ya mpakani
Thailand na Cambodia zimekuwa zikishambuliana vikali katika maeneo kadhaa ya mpaka wao wenye urefu wa kilomita 817 tangu Jumatatu.
Mapigano hayo yameibuka baada ya utulivu wa muda tangu mapambano makali ya siku tano ya mwezi Julai yaliyokwisha baada ya Marekani na Malaysia kufanya ususulhishi. Tangu mzozo wa awamu hii ulipoibuka kati ya nchi hizo za Asia, wanajeshi 14 wa Thailand na raia 11 wa Cambodia wameuawa kwa mujibu wa mamlaka za mataifa hayo.