1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yakasirishwa na Marekani

Daniel Gakuba
4 Julai 2018

Sudan imepinga maelekezo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani yakiwataka raia wake kutofanya ziara nchini Sudan kwa hoja kwamba makundi ya kigaidi yalikuwa yakipanga mashambulizi dhidi ya wageni.

https://p.dw.com/p/30pNU
Suadan Präsident Omar Al Bashir
Picha: Reuters/M. Abdallah

Maelekezo hayo yaliyochapishwa jana kwenye tovuti ya ubalozi wa Marekani mjini Khartoum, yamekuja siku chache baada ya Marekani kuondoa vikwazo vya kibiashara ilivyoviweka dhidi ya Sudan mwaka 1997.

Wizara ya mambo ya nje mjini Washington imesema katika maelekezo hayo kwamba makundi ya kigaidi yalikuwa yakijipanga kuwashambulia wageni hususan mjini Khartoum, na pia katika majimbo mengine matatu yenye mizozo, ambayo ni Darfur, Blue Nile na Kordofan ya Kusini.

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema maelekezo hayo ya Marekani yanakwenda kinyume na mtazamo wa Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya nchi za Kiarabu, jumuiya ambazo kwa mujibu wa wizara hiyo zimeelezea mazingira nchini Sudan kuwa ya utulivu.