Miezi miwili iliyopita, kamera za televisheni ziliuonyesha ulimwengu maandamano ya watu wenye sera kali za kuwapinga wageni wakiandamana kwa hasira katika mji wa Chemnitz Mashariki mwa Ujermani. Alhamis, Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliuzuru mji huo, kuzungumza na wakazi wake, akiwa na ujumbe mmoja: Tunahitaji kuzungumza. Sikiliza ripoti ya Jacob Safari kujua mengi zaidi.