1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

25.04 Siku ya Malaria Duniani

25 Aprili 2023

Leo Aprili 25, Ulimwengu unaadhimisha siku ya kupambana na ugonjwa wa Malaria.

https://p.dw.com/p/4QWb6
Äthiopien | Logo World Malaria Day
Picha: Southern Regional Health Bureau

Katika jimbo la kivu kusini Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lenye zaidi ya watu millioni moja wanaougua ugonjwa wa malaria, na licha ya hatari ya wazi ya ugonjwa huo, baadhi ya wakaazi wanasusia kulala ndani ya neti za kujikinga na mbu.

Ugonjwa wa malaria unatakiwa kutibiwa bila malipo katika miundo ya afya nchini Congo, japo hali haiko hivyo.

Katika vituo vya afya wagonjwa wanapewa ushauri, uchunguzi wa haraka na dawa ambazo serikali na washirika wake hutoa kwa wagonjwa baada ya wagonjwa kulipa, kama inavyoonekana.

Hali ya kupuuzwa kwa Malaria

Malariabekämpfung in Sambia
Kampeni ya kupiga vita malaria ZambiaPicha: picture-alliance/ dpa

Christine Mujijima ni mkazi wa Kivu kusini, anahisi kwamba malaria imegeuzwa kuwa kama ugonjwa wa kawaida.

Mpango wa Kudhibiti Malaria wa idara ya afya Kivu kusini unazidi kueleza wasiwasi kuhusu ongezeko la kiwango cha maambukizi ya malaria katika jimbo la Kivu Kusini.

Kulingana na mpango huo, katika idadi ya wakazi elfu moja, mia mbili kati yao ni wanaugua malaria. Hata hivyo, inavyoonekana ni kwamba baadhi ya wakaazi hawatumi neti za kujikinga na mbu, na wengine wanazitumia kwa ajili ya shughuli zingine.

Watoto na kina mama ni waathirika zaidi

Idara ya afya katika jimbo la Kivu kusini imebaini kwamba watoto wachanga hadi wenye umri wa miaka mitano pamoja na wanawake wajawazito ndio wanaoathirika zaidi. Mpango huo wa serikali ya Congo unasisitiza matumizi sahihi ya neti zilizotiwa dawa na kudumisha usafi wa mazingira, kama njia muhimu ya kupambana na kuenea kwa Malaria.

Pia, mamlaka ya afya inaendelea kuhimiza wakaazi kuhusu uhifadhi wa mazingira ili kupambana na maji yanayotuama huku na kule mitaani yakisababisha ongezeko la mbu. Daktari Stephane Mukendi ni msimamizi wa tume ya kutoa huduma za afya mjini Kinshasa, anaeleza juhudi zinazofanyika kwa kusema "Tayari tunachofanya hapa sasa pia ni juhudi, yaani Uhamasishaji huu ili watu wajue kuwa malaria ilikuwepo na kwamba inaendelea katika jamii yetu, na kisha kuna programu ambayo itaonyesha hatari ya kuambukizwa kwa pamoja kwa malaria na magonjwa mengine, na utambuzi tofauti”.

Soma zaidi:Nigeria yatoa idhini ya matumizi ya chanjo ya Malaria kutoka Chuo Kikuu cha Oxford

Maeneo yanayozidi kuathirika zaidi ni yale ya karibu na ziwa Kivu na Tanganyika. Mamlaka husika inalenga kuongeza juhudi za kusambaza neti za kujikinga na mbu katika maeneo hayo licha ya changamoto za kifedha.

Mitima Delachance, DW, Bukavu