Sherehe za Muungano wa Ujerumani zaendelea | NRS-Import | DW | 03.10.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Siasa

Sherehe za Muungano wa Ujerumani zaendelea

Sherehe za miaka 26 tangu Ujerumani illipoungana upya zinafanyika mwaka huu katika mji wa mashariki wa Dresden. Mbali na shamra shamra na burudani ya siku tatu ,ibada maalum inafanyika katika kanisa la Frauenkirche

Miongoni mwa wageni rasmi katika kanisa la Frauenkirche ni pamoja na kansela Angela Merkel,rais wa shirikisho Joachim Gauck na mwenyekiti wa korti ya katiba Andreas Voßkuhle. Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili katika jimbo la Saxony Carsten Rentzing akihubiri mbele ya watu zaidi ya 1200 waliohudhuria hafla hiyo katika kanisa la Frauenkirche amekumbusha umuhimu wa amani akisema haiji hivi hivi anasisitiza kwa kusema amani "inabidi ipaliliwe na kutunzwa kila siku."Yangetokea mengi ya maana kama tungejiuliza masuala yanayozusha wasi wasi katika jimbo letu,kuhusu namna ya kutafuta na kupata amani" ameongeza kusema askofu mkuu wa jimbo la Saxony Carsten Rentzing na kushadidia tunanukuu: "Amani inapindukia makubaliano ya kuweka chini silaha,amani inamaanisha pia haki na uhuru. Ndio maana anasema ni muhimu masuala kama hayo watu kujiuliza siku kama hii ya Oktober tatu-siku ya kutafakari na kujidadisi."

Hofu za machafuko wakati wa sherehe za muungano Dresden

Maandamano ya wafuasi wa Pegida

Maandamano ya wafuasi wa Pegida

Sherehe za mwaka huu zinafanyika katika hali ya tahadhari; hatua za usalama zikiimarishwa. Licha ya hatua hizo kali za usalama mamia ya waandamanaji walianza kuwazomea na kufika hadi ya kuwatukana wageni wanaohudhuria sherehe za muungano. Waandamaji hao ambao wengi wao ni wafuasi wa  vuguvugu linalopinga wageni-Pegida wamekuwa wakipaza sauti wakiwakaripia wanasiasa wanaohudhuria sherehe hizo na kuwaita wasaliti. Watu zaidi ya laki saba na nusu wanatazamiwa kuhudhuria sherehe mbali mbali ;kauli mbiu ikiwa jenga daraja".Pegida wanapanga kuendelea pia na maandamano yao ya kila jumatatu. Wafuasi wasiopungua elfu tatu wa kundi hilo wanatarajiwa kushiriki. Na makundi mengine yanayopalilia chuki dhidi ya wageni yanapanga pia kuteremka majiani leo usiku. Mahmnut Bacaru ni mkaazi wa Dresden:"NNaishi Dresden tangu miaka 20 iliyopita,sijawahi kuona mambo kama haya. Dresden ni mji wa kuvutia kupita kiuasi-kwanini baadhi ya watu wanataka kuufuja?Sijawahi mie kuona haya yanayotokea na sitaki kuona yakitokea tena."

 Sherehe za muungano zinaendelea

Sherehe za miaka 26 ya Muungano

Sherehe za miaka 26 ya Muungano

Hivi punde kansela Angela Merkel,rais wa shirikisho,Joachim Gauck,spika wa bunge la shirikisho,Norbert Lammert pamoja pia na wawakilishi wa serikali kuu na serikali za majimbo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe rasmi katika ukumbi wa michezo ya kuigiza wa Samperoper.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/epd

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com