1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shambulizi la Israel nchini Lebanon lawaua watu watatu

17 Mei 2024

Idadi ya waliofariki baada ya shambulizi la Israel nchini Lebanon imefikia watu watatu na watu wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya. Haya ni kwa mujibu wa vyanzo nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/4g0hK
Askari wa israel wakipiga doria karibu na mpaka na Lebanon
Askari wa israel wakipiga doria karibu na mpaka na LebanonPicha: Francisco Seco/AP/picture alliance

Idadi ya waliofariki baada ya shambulizi la Israel nchini Lebanon imefikia watu watatu na watu wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya. Haya ni kwa mujibu wa vyanzo nchini Lebanon.Je Syria ndio sababu ya Iran na Israel kushambuliana?

Vyanzo hivyo vimesema kuwa mfuasi mmoja wa kundi la wanamgambo la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran na wafanyakazi wawili wa Syria waliuawa katika shambulio hilo la leo kusini mwa mji wa Pwani wa Sidoni nchini Lebanon ulio umbali wa kilomita 55 kaskazini mwa mpaka wake na Israel.

Hezbollah imethibitisha kifo hicho cha mfuasi wake lakini haikusema ni lini, wapi na aliuawa kwa namna gani.Israel yamuuwa kamanda katika shambulizi Lebanon

Jeshi la Israel pia limethibitisha kutokea kwa shambulio hilo na kusema lililenga kituo cha ulinzi wa anga cha Hezbollah kilichokuwa kitisho kwa ndege za kivita za Israel.

Kulingana na ripoti za jeshi hilo, awali, eneo la kaskazini la Israel lilishambuliwa kwa droni.