1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la Israel lawauwa watu sita Gaza

14 Machi 2026

Shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limesema leo kuwa mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya watu sita katika muda wa saa 24 zilizopita.

https://p.dw.com/p/5AP9c
Gaza City 2026
Wapalestina wakagua hasara ya shambulizi la Israel Gaza City mnamo Januari 31, 2026Picha: Majdi Fathi/NurPhoto/picture alliance

Shirika hilo la ulinzi wa kiraia la Gaza, limesema kuwa wakati wa shambulizi hilo lililotokea leo alfajiri,  polisi wawili na raia mmoja waliuawa katika mji wa kusini wa Khan Yunis.

Pia limesema kuwa shambulizi la jana jioni dhidi ya kundi la raia mashariki mwa Gaza City lilisababisha vifo vya watu watatu ambao miili yao ilipelekwa katika hospitali kuu ya eneo hilo Al- Shifa.

Hata hivyo jeshi la Israel halikujibu ombi la tamko kuhusu tukio hilo.