1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudia na Qatar zapongeza utambuzi wa dola la Palestina

22 Mei 2024

Saudi Arabia na Qatar zimepongeza uamuzi wa Ireland, Norway na Uhispania wa kuitambua Palestina kama dola huru na kutoa wito kwa mataifa mengine kuchukua hatua kama hiyo.

https://p.dw.com/p/4g9Wl
Waandamanaji wa Ujerumani wanaounga mkono Palestina Berlin
Watu wakiwa na bendera ya Palestina wakati wa maandamano ya mshikamano na Palestina huko Berlin Novemba 4, 2023.Picha: Emmanuele Contini/IMAGO

Saudi Arabia imekuwa ikiunga mkono hatua hiyo na kamwe haijawahi kuitambua Israel kama dola, japo mwezi Septemba mwanamfalme ambaye ndie mtawala wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman alisema hatua zimepigwa pamoja na Marekani, kuhusu makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kidiplomasia, yanayoweza pia kuhusisha hatua ya kuimarisha usalama na masuala mengine

Qatar imesema imekaribisha uamuzi wa kuitambua Palestina kama dola huru, ikisema ni  hatua muhimu kuelekea suluhu ya madola mawili.

Jordan na Baraza la ushirikiano la nchi za Ghuba GCC pia zimepongeza uamuzi huo zilizouita wa kihistoria, huku Ujerumani kupitia msemaji wake wa masuala ya nje ikisisitiza uwepo wa suluhu ya madola mawili lakini ikatahadharisha kua lazima kuwepo na mazungumzo kabla ya hilo kufanyika.