Roma: Italia na kujiuzulu kwa Prodi | Habari za Ulimwengu | DW | 22.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Roma: Italia na kujiuzulu kwa Prodi

Roma:

Rais Giorgio Napolitano wa Italia atakua na mazungumzo na Viongozi wa kisiasa hii leo, kuona kama Waziri mkuu Romano Prodi aliyejiuzuluu baada ya miezi tisa madarakani anaweza bado kuunda serikali mpya. Prodi alijiuzulu baada ya serikali yake ya mrengo wa kati wa bawa la shoto,kushindwa kwa kura chache katika mswaada uliowasilishwa katika baraza la Seneti juu ya sera ya nje. Hayo ni pamoja na kuongezwa wanajeshi karibu 2,000 wa Kitaliani nchini Afghanistan na kuidhinishwa utanuzi wa kambi ya kijeshi ya Marekani katika mji wa Vacenza , kaskazini mwa Italia. Bado haijafahamika iwapo Rais Napolitano ataukubali uamuzi wa kujiuzulu Waziri mkuu Prodi. Kwa wakati huu serikali yake imeombwa kuendelea madarakani kama serikali ya muda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com