1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Macron mwenyeji wa mkutano wa kujadili kadhia ya Ukraine

26 Februari 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakuwa mwenyeji wa viongozi wa dunia mjini Paris kwa ajili ya mkutano wa kuimarisha uungwaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4csD1
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakibadilishana hati baada ya kutia saini makubaliano
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakibadilishana hati baada ya kutia saini makubalianoPicha: Thibault Camus/AP Photo/picture alliance

Ofisi ya Macron imetangaza kuwa mkutano huo utawapa washiriki nafasi ya kuonyesha umoja pamoja na azma yao ya kuishinda Urusi.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Rais wa Poland Andrzej Duda, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte pamoja na viongozi wa mataifa ya ukanda wa Skandinavia na Baltic watakuwa miongoni mwa viongozi 20 watakaodhuria mkutano huo.

Marekani, Uingereza na Canada watatuma wanadiplomasia wa ngazi ya juu kwenye mkutano huo. Hata hivyo, hakuna wawakilishi kutoka India au China watakaohudhuria.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ataufungua mkutano huo kwa kutoa hotuba kwa njia ya vidio.