Putin asema Urusi inashirikiana na Marekani kuhusu Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Putin asema Urusi inashirikiana na Marekani kuhusu Syria

Rais Vladimir Putin amesema majeshi ya Urusi yanawapa ulinzi wa anga ,baadhi ya wapinzani nchini Syria, wanaopambana na magaidi wa dola la Kiislamu

Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza na waandishi wa habari mjini Moscow

Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza na waandishi wa habari mjini Moscow

Rais Putin alisisitiza kwenye mkutano na waandishi wa habari , unaofanyika kila mwaka, kwamba Urusi inashirikiana na Marekani nchini Syria.

Hata hivyo kwa mara nyingine aliinawa Uturuki na kusema kuwa serikali ya nchi hiyo inajikomba kwa Marekani . Amesema haoni iwapo pana uwezekano wa kuufanya uhusiano baina ya Urusi na serikali ya Uturuki uwe mzuri.

Putin amefahamisha kuwa Urusi inawasiliana na baadhi ya wapinzani wa Syria lakini bila ya kuwataja wapinzani hao.

Kiongozi huyo wa Urusi anaeitwa mwamba, na vyombo vya habari vya magharibi, aliitumia fursa ya mkutano na waandishi wa habari mjini Moscow kusisitiza kwa mara nyingine kwamba mashambulio ya ndege za Urusi yanawalenga magaidi wa dola la kiislamu, kinyume na madai yanayotolewa na nchi za magharibi kwamba Urusi inawashambulia wapinzani wa Assad.

Rais wa Syria Bashar al-Assad akihojiwa

Rais wa Syria Bashar al-Assad akihojiwa

Putin ameeleza kuwa inawezekana kuleta suluhisho la kisiasa nchini Syria. Lakini amesisitza kuwa ni watu wa Syria tu wenye haki ya kuchagua wa kuwaongoza.

Rais Vladimir Putin ameyatamka hayo siku moja kabla ya kufanyika, mjini New York kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 17, ikiwa pamoja na kutoka Urusi,Iran na Saudi Arabia zinazohesbaika kuwa na uzito wa juu katika mgogoro wa nchini Syria.

Mawaziri hao watakutana kwa ajili ya duru ya tatu ya mazungumzo juu ya kuumaliza mgogoro wa Syria. Kwenye mkutano wao wa hivi karibuni, mawaziri hao walikubaliana juu ya kufanyika mazungumzo ya amani , yatakayoongozwa na Umoja wa Mataifa na ikiwezekana kusimamisha mapigano mnamo mwezi wa Januari.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kuwasilisha mswada wa azimio juu ya kuzifunga njia za kuingizia fedha zinazotumiwa magaidi wa dola la kiislamu .Putin ameahidi kuwa Urusi itauunga mkono mswada huo.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mjini Moscow Rais Putin pia alizungumzia juu ya masuala ya FIFA, na kampeni za kuwania nafasi ya kugombea urais nchini Marekani.

Mwandishi:Mtullya Abdu./afp,

Mhariri:Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com