Putin amsifu Al Sharaa kwa kurejesha uthabiti Syria
28 Januari 2026
Matangazo
Putin ametoa pongezi hizo kwa al-Sharaa ambaye yuko ziarani Urusi kwa mara ya pili tangu Bashar al Assad alipong'olewa madarakani. Aidha Rais wa mpito wa Syria kwa upande wake amemshukuru Putin kwa msaada wake katika kuimarisha hali ya Syria na ukanda wote.
Mazungumzo kuhusu kambi za kijeshi za Urusi
Ziara yake Moscow, inalenga kufanya mazungumzo yatakayojikita katika mustakabali wa kambi za kijeshi za Urusi nchini Syria. Kwa Urusi, ni muhimu kuendelea kuwa na kambi za kijeshi katika Pwani ya Syria ili kuendeleza uwepo wa jeshi lake kwenye eneo la Mediterania.