Putin aingilia kati mvutano wa Iran na Israel
16 Januari 2026
Matangazo
Kremlin imesema Putin amezungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, akisisitiza umuhimu wa kupunguza mvutano. Putin pia ameahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Iran, huku Tehran ikishukuru Urusi kwa kuiunga mkono katika Umoja wa Mataifa.
Wachunguzi huru wanasema maelfu wameuawa na vikosi vya usalama vya Iran katika ukandamizaji mkali wa maandamano ya kupinga serikali, hali iliyochochea vitisho vya hatua za kijeshi kutoka Marekani, mshirika mkuu wa Israel.
Huku haya yakijiri maandamano nchini Iran yanaonekana kupungua kutokana na ukandamizaji mkali na kuzimwa kwa mtandao kwa zaidi ya wiki moja.