PARIS:Sudan kuwekewa vikwazo na Ufaransa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS:Sudan kuwekewa vikwazo na Ufaransa

Rais wa Ufaransa Jacques Chirac anatoa wito kwa nchi ya Sudan kuwekewa vikwazo endapo visa vya uhalifu dhidi ya ubinadamu vinaendelea katika eneo linalokumbwa na vita la Darfur.Kulingana na kiongozi huyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halina budi ila kuwachukulia hatua ya kuwawekea vikwazo endapo makubaliano hayataheshimiwa na serikali ya Sudan.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa liliidhinisha azimio la kuepeleka kikosi cha majeshi ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa cha kulinda amani katika eneo la Darfur ili kuimarisha majeshi ya Umoja wa Afrika yaliyoko kwa sasa yanayokumbwa na uhaba mkubwa wa vifaa.Rais wa Sudana Omar al Bashir kwa sasa anakataa kuidhinisha utekelezaji wa hatua hiyo aliyokubali mwezi Novemba mwaka jana.

Mapigano kati ya waasi na wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali yamesababisha vifo vya watu laki mbili na kuacha wengine zaidi ya milioni mbili bila makao katika eneo la Darfur.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com