1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVatican

Papa Leo alaani waziwazi hali ya Wapalestina huko Gaza

25 Desemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV, katika hotuba yake ya kwanza ya Krismasi maarufu kama "Urbi et Orbi" amelaani hadharani hali wanayoishi Wapalestina huko Gaza.

https://p.dw.com/p/55y7V
Vatican 2025 | Papa Leo XIV
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIVPicha: Yara Nardi/REUTERS

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV, katika hotuba yake ya kwanza ya Krismasi aliyoitoa kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro na isiyo ya kawaida kwa ibada ambayo wakati wote huwa ya kiroho na tulivu pia amelaani mateso ya watu wasio na makazi duniani na uharibifu unaosababishwa na vita.

Papa Leo amesema maisha ya raia wasio na ulinzi, hususan vijana wanaolazimishwa kubeba silaha, miili yao dhaifu huachwa na majeraha ya kudumu.

Katika ibada hiyo ya ujumbe wa baraka kwa nchi, miji na ulimwengu mzima,  kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Leo, ametoa mwito wa kukomeshwa vita vinavyondelea kokote duniani.