1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV aonya kuhusu mizozo duniani

27 Novemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo wa 14 amelalalamikia mizozo iliyotawaliwa na umwagaji damu inayoendelea duniani na kusema kuwa inahatarisha mustakabali wa ubinadamu.

https://p.dw.com/p/54Oam
Ankara, Uturuki  Novemba 27, 2025
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV na Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Umit Bektas/REUTERS

Papa Leo ameeleza kuwa dunia inayumba kutokana na tamaa na kuchagua mambo yanayodidimiza haki na amani. Ameyasema hayo akiwa ziarani Uturuki ambako amekutana na kuzungumza na Rais Recep Tayyip Erdogan.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani pia ameitolea wito Uturuki kulifurahia jukumu lake kama msuluhishi wa mataifa  katika juhudi za kutafuta amani ya kudumu.

Erdogan ausifu msimamo wa Papa Leo juu ya Palestina

Kwa upande wake Rais Erdogan ameusifu msimamo wa Papa Leo kuhusu suala la Palestina baada ya mkutano wao. Erdogan amesema ana matumaini kuwa ziara hiyo ya kwanza ya Kimataifa ya Papa, itakuwa ya manufaa kwa utu wakati kukiwa na mivutano na hali ya mashaka ulimwenguni.