1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo aitaka Mashariki ya Kati iachane na ukatili wa vita

2 Desemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amekamilisha ziara yake nchini Lebanon leo kwa kutoa mwito kwa viongozi kote Mashariki ya Kati, kuvisikiliza vilio vya aman vya raia wao.

https://p.dw.com/p/54deA
Libanon Beirut 2025 | Papst Leo XIV. verlässt den Libanon
Picha: Ibrahim Amro/AFP/Getty Images

Papa Leo amewataka viongozi hao waubadilishe mwenendo wao na waachane na ukatili wa mapigano.

Papa ameyasema hayo alipouhutubia umati wa watu laki moja na nusu wakati wa misa takatifu huko mjini Beirut.

Ameusihi uongozi wa Lebanon pia kutafuta suluhu la miaka ya machafuko, migogoro ya kisiasa na uchumi uliosambaratika.

Amesema eneo zima la Mashariki ya Kati linahitaji mwongozo mpya ili kukuishinda migawanyiko ya kisiasa, kijamii na kidini.

Kiongozi huyo wa kidini amekuwa katika mkumbo wa pili wa ziara yake ya siku tatu nchini Uturuki na Lebanon.