1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Imani

Papa Leo atembelea Msikiti wa Bluu mjini Istanbul

29 Novemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ameendelea na ziara yake leo nchini Uturuki kwa kutembelea Msikiti wa Bluu mjini Istanbul.

https://p.dw.com/p/54TqG
Türkiye Istanbul 2025 | Papa Leo XIV atembelea Msikiti wa Bluu (Msikiti wa Sultan Ahmed)
Papa Leo XIV atembelea Msikiti wa Bluu (Msikiti wa Sultan Ahmed)Picha: Vatican Media/ZUMA/picture alliance

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ameendelea na ziara yake leo nchini Uturuki kwa kutembelea Msikiti wa Bluu mjini Istanbul.

Papa Leoalikuwa akifuata nyayo za watangulizi wake ambao wote walifanya ziara ya ngazi ya juu katika msikiti huo, katika ishara ya heshima kwa jamii ya Waislamu walio wengi nchini Uturuki.

Kabla ya kuingia Msikitini, Papa Leo alivua viatu na kuinama kidogo, kisha kutembezwa na Imamu wa Msikiti na Mufti wa Istanbul ndani ya msikiti huo unaowakusanya Waumini wapatao 10,000. Hii ni ziara ya kwanza ya kigeni kwa Papa Leo tangu aingie madarakani ambapo pia anatazamiwa kuzuru Lebanon.

Papa huyo wa kwanza mwenye asili ya Marekani, anatarajiwa kuzungumza kwa mapana juu ya amani ya Mashariki ya Kati.