Niersbach: Ujerumani inaweza kutwaa ubingwa | NRS-Import | DW | 25.06.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Niersbach: Ujerumani inaweza kutwaa ubingwa

Matumaini ya kufanya vyema katika michuano ya kombe la kandanda la dunia kwa timu ya taifa ya Ujerumani sio tu yapo kwa mashabiki wa soka wa nchi hiyo bali hata kwa wadau wengine

Rais wa chama cha soka cha Ujerumani Wolfagang Niersbach anakiri kufurahishwa kwa kuanza vizuri kwa miamba hiyo ambayo iliichara Ureno goli nne kwa bila kisha ikaenda sare ya goli mbili kwa mbili dhidi ya Ghana.

Niersbach anasema anahisia sawa na mashabiki waliojitokeza mitaani kushangilia ushindi dhidi ya Ureno kwani hakutarajia kuanza vizuri kiasi kile katika michuano ya kombe la dunia tena dhidi ya timu inayoshika nafasi ya tatu katika orodha ya viwango vya ubora ya shirikisho la kandanda duniani FIFA.

Deutschland Fußball Nationalmannschaft Abwehr Mats Hummels Benedikt Höwedes und Per Mertesacker

Vijana wa Ujerumani wanatarajiwa kufika katika fainali

"Ilikuwa ni kidogo kama mchezo dhidi ya Yugoslavia katika fainali za mwaka 1990 mjini Milan, hivi karibuni nimempigia Franz Backenbauer nae anafikiria hivyo hivyo" alisema Niersbach.

Niersbach anaongeza na kusema kuna vitu vinavyofanana na wakati ule kwasababu Ujerumani ilikabiliana na timu imara na nafasi ya kila timu kushinda ilikuwa ni 50/50 hivyo wengi hawakujua timu yao itachezaje.

Rais huyo wa shirikisho la soka la Ujerumani anasema hakuna shaka kwamba uwezo na ari uliooneshwa na timu hiyo utaisaidia kufika mbali katika mashindano hayo.

Kuhusiana na msisimko wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil, Niersbach anasema alipata bahati ya kuwepo katika jiji la Sao Paulo mapema wakati michuano hiyo ilipoanza na anakiri kuwa kulikuwa hakuna ishara ya vitu ambavyo vinaashirikia mji huo utakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia kama ilivyokuwa katika fainali za mwaka 2006 ambazo Ujerumani iliandaa, lakini Niersbach anasema ndani ya viwanja kuna msisismko wa kutosha ambao unafanya fainali za mwaka huu kuwa na mvuto wa aina yake.

Mwandishi: Anuary Mkama/DW
Mhariri: Bruce Amani

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com