1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa Kijerumani awauwa watu wanne kwa risasi

John Juma
1 Machi 2024

Mwanajeshi mmoja wa Ujerumani anashukiwa kuwapiga risasi na kuwauwa watu wanne usiku wa kuamkia Ijumaa (Machi 1) katika wilaya ya Rotenburg jimbo la Lower Saxony, kisha akajisalimisha kwa maafisa wa polisi na kushtakiwa.

https://p.dw.com/p/4d5Sp
Bundeswehr
Askari wa jeshi la Ujerumani, Bundeswehr.Picha: picture alliance/dpa

Miongoni mwa waliouawa kwenye mashambulizi hayo ni mtoto mdogo.

Wachunguzi hawakutoa maelezo zaidi kuhusu waathirika wa tukio hilo, kama vile umri, jinsia au uhusiano wao na mshukiwa.

Mshukiwa wa uhalifu huo alijisalimisha baada ya shambulizi hilo na kukamatwa, wachunguzi walisema.

Polisi walisema mivutano ya ndani ya nyumba inaweza kuwa sehemu ya uchunguzi wao kwenye chanzo cha uhalifu huo.