1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati maarufu Jesse Jackson afariki dunia

17 Februari 2026

Jesse L Jackson amefariki leo Jumanne akiwa na umri wa miaka 84 nyumbani kwake akizunguukwa na wanafamilia.

https://p.dw.com/p/58vUl
Jesse Jackson alipowahi kukutana na hayati aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela
Jesse Jackson alipowahi kukutana na hayati aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson MandelaPicha: Jon Hrusa/dpa/picture alliance

Mwanaharakati na mwanasiasa wa miaka mingi aliyewahi kugombea mara mbili kiti cha urais nchini Marekani Mchungaji Jesse L Jackson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

Jesse Jackson aliyefariki nyumbani kwake akiwa amezungukwa na familia yake, anakumbukwa kwa kuongoza kwa miongo kadhaa vuguvugu la harakati za kutetea haki za kiraia nchini Marekani baada ya kuuwawa kwa mwanaharakati Martin Luther King Jr. Viongozi mbalimbali waomboleza kifo cha Winnie Mandela

Jackson aliongoza mihadhara ya dini ya kikristo ndani na nje ya Marekani akipambania watu masikini na waliotengwa kwenye jamii katika masuala ya haki ya kupiga kura na elimu na afya.