1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwalimu wa Ujerumani anayetembelea nchi za wanafunzi wake

Grunau Andrea/Hamidou Oummilkheir5 Machi 2019

Jan Kammann ambaye ni mwalimu wa shule nchini Ujerumani, hutembelea nchi ambako wanafunzi wake wanatokea, kwa lengo la kujua wanakotoka na hali yao ya maisha ikiwemo changamoto wanazopitia.

https://p.dw.com/p/3EUEH
Lehrer Jan Kammann
Picha: Jan Kammann und Luisa Wolff

Mwalimu wa shule nchini Ujerumani aliyeamua kuuzunguka ulimwengu kuzitembelea nchi ambako wanafunzi wake wanatokea. Jan Kammann ameshafika Kosovo, Iran ambako alikutana na watoto kutoka Afghanistan, amewatembelea wanafunzi nchini Ghana, amekwenda Korea ya Kusini ambako amejifunza kupika na kufika hadi ya kuutembelea msitu mweusi nchini Nicaragua. 

Tangu miaka sita iliyopita mwalimu wa lugha ya kiiengereza na fani ya jiografia, Jan Kammann, mwenye umri wa miaka 39 amekuwa akisomesha katika shule ya sekondari ya Hamm mjini Hamburg. Shule hiyo ya Ulaya yenye nembo inayoshadidia "mshikamano katika mchanganyiko wa makabila tofauti" ina wanafunzi wake kwa waume kutoka kila pembe ya dunia. Wanafunzi hao na wazee wao wamekuja Ujerumani kutokana na sababu tofauti: wamekuja kama wakimbizi, au wamekuja kwa ajili ya kusoma kwa sababu wazee wao wanafanyakazi au kwa sababu watoto wanasoma katika shule moja mashuhuri ya ngoma ya baleti au ngoma ya kuigiza hadithi.

Miongoni mwa nchi ambazo Jan Kammanns ametembelea ambako wanafunzi wake hutokea ni pamoja na Kosovo, Iran, China, Ghana, Korea Kusini na hata kujifunza kupika vyakula vyao.
Miongoni mwa nchi ambazo Jan Kammanns ametembelea ambako wanafunzi wake hutokea ni pamoja na Kosovo, Iran, China, Ghana, Korea Kusini na hata kujifunza kupika vyakula vyao.Picha: Jan Kammann und Luisa Wolff

Jan Kammann amechapisha kitabu kinachozungumzia shida wanazokabiliana nazo wanafunzi hao wanapokuwa ndio kwanza wanajiunga na shule yake. Anasema kinakuwa kishindo kwa sababu si wanafunzi na wala si wazee wao hakuna anaezungumza Kijerumani. Kwa hivyo wanajikuta katika hangaiko la jinsi ya kujiunga na maishab ya kila siku ya jamii .Katika nchi nyengine mengi ni tofauti,Na ili kuwaelewa vyema wanafunzi wake Jan Kammann ameamua kuchukua likizo bila ya malipo kwa muda wa mwaka mmoja na kuzitembelea nchi wanafunzi wake wanakotokea tangu barani Ulaya, Asia, Latin America na barani Afrika. Ameandika kitabu kuhusu ziara yake hiyo:"Darasa la Kijerumani, wanafunzi 30, mataifa 22, nchi 14 na mwalimu mmoja anaeizunguka dunia."

Akiulizwa na DW kuhusu kitabu chake, amefafanua kwa kusema: "Kwanza naona picha mbele yangu ya jinsi wanafunzi, wake kwa waume na wazee wao wanavyojikuta katika hali ya hangaiko wanapokuja katika shule zetu. Si wazee na wala si watoto, hakuna anaezungumza kijerumani na wanabidi wajitolee. Hisia hizo za kujikuta unajitolea mtu anabidi kwanza azielewe na kuziishi. Mimi kilichonisaidia zaidi ni yale maarifa niliyoyapata. Niliwahi kujikusanyia maarifa kama hayo nilipokuwa China.

Jan Kammanns hutembelea nchi ambako wanafunzi wake hutoka ili kuelewa shida ambazo huwakabili.
Jan Kammanns hutembelea nchi ambako wanafunzi wake hutoka ili kuelewa shida ambazo huwakabili.Picha: Jan Kammann und Luisa Wolff

Ni kitu ambacho mtu anaweza kukilinganisha na hangaiko la kila siku la maisha. Matokeo yake ndio hayo. Lakini kwengineko matokeo ni tofauti na hilo ni muhimu zaidi kwangu mie, kuona mtu anakuwa na hisia ya kutojua kitu, anajiuliza niko wapi mie, nnakutwa na nini na licha ya hayo akawa na imani na watu anaokutana nao. Pengine kwa tabasamu akatamka "Hallo". Inasaidia sana, kwa sababu hali kama hii ni ngumu kwa kila mmoja, tangu wanafunzi, wazee na kadhalika. Mambo mengi yanategemea hali hiyo.

Tangu alipofanya ziara hiyo mwalimu Jan Kammann amefumbuka macho na kuwathamini zaidi wanafunzi wake kwa bidii yao ya kujifunza kijerumani na akujiambatanisha na utaratibub wa maisha humu nchini.