1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muigizaji wa filamu wa Marekani Chuck Norris afariki

20 Machi 2026

Muigizaji filamu za kivita wa Marekani na nyota wa Hollywood Chuck Norris ameaga dunia. Norris amefariki akiwa na umri wa miaka 86.

https://p.dw.com/p/5AnzM
Nyota wa Hollywood Chuck Norris amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.
Nyota wa Hollywood Chuck Norris amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.Picha: Frazer Harrison/Getty Images

Chuck Norris, muigizaji filamu za kivita wa Marekani na nyota wa Hollywood maarufu kwa uigizaji wake katika "Walker, Texas Ranger," amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 86.

Familia yake imesema katika taarifa kwenye Instagram hivi leo kwamba ni kwa mioyo mizito ambapo wanatangaza kifo cha ghafla cha mpendwa wao Chuck Norris kilichotokea jana asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo familia imesema aliishi maisha yake kwa imani, kusudi, na kujitolea bila kuyumba kwa watu aliowapenda. Kupitia kazi yake, nidhamu, na wema, aliwatia moyo mamilioni duniani kote na kuacha athari ya kudumu kwa maisha mengi.

Inaripotiwa Chuck Norris kuwa aliugua Alhamisi katika kisiwa cha Hawaii cha Kauai.