1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu aliyemshambulia mume wa Nancy Pelosi afungwa miaka 30

18 Mei 2024

Mahakama nchini Marekani imemuhukumu miaka 30 jela mwanaume mmoja aliyemshambulia kwa nyundo mume wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi.

https://p.dw.com/p/4g1XP
US Nancy Pelosi
Picha: Carolyn Kaster/AP/picture alliance

Tukio hilo lilifanyika mnamo mwezi Oktoba mwaka 2022. David DePape aliyemshambulia mume wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelocy alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuingia kinyume cha sheria kwenye nyumba ya wanandoa hao mjini San Francisco na kumshambulia Paul Pelosikatika shambulio la kutisha lililonaswa na kamera za usalama.

Awali, waendesha mashtaka walikuwa wameiomba mahakama ya shirikisho huko San Francisco kumhukumu DePape kifungo cha miaka 40 jela. Watu wengine ambao mshtakiwa huyo alikiri kutaka kuwashambulia ni pamoja na Gavana wa California Gavin Newsom, mtoto wa Rais Joe Biden, Hunter Biden, na mwigizaji Tom Hanks.