1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Mtihani kwa ANC katika uchaguzi wa kitaifa Jumatano

28 Mei 2024

Raia wa Afrika Kusini wanapiga kura 29.05.2024 Jumatano kuchagua bunge jipya.

https://p.dw.com/p/4gNgO
 WAfrika Kusini kupiga kura Jumatano kuchagua bunge jipya
WAfrika Kusini kupiga kura Jumatano kuchagua bunge jipyaPicha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Uchaguzi huo utakuwa wa saba wa kidemokrasia tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mnamo mwaka 1994 wakati Nelson Mandela alipochaguliwa kuwa rais huku chama tawala ANC wakati huo kikijizolea asilimia 62.5 ya kura.

Hata hivyo, baada ya miaka 30 ya uongozi, chama tawala ANC kinakabiliwa na upinzani mkubwa huku kikihitaji asilimia 50 ya kura ili kuendeleza wingi wake wa viti bungeni.

Ufisadi, kutetereka kwa uchumi na ukosefu wa ajira ni baadhi tu ya masuala yanayowaathiri raia nchini humo.

Rais Cyril Ramaphosa amekabiliwa na wakati mgumu kuinua uchumi wa taifa hilo huku thuluthi moja ya Waafrika Kusini wakikosa ajira.

Wapiga kura huenda wakatumia sababu hizo kukiadhibu chama cha ANC kwenye uchaguzi huo.