MOSCOW: Mwandishi habari Anna Politkovskaya akumbukwa nchini Urusi
7 Oktoba 2007Matangazo
Wanaharakati kadhaa wanaotetea haki za binadamu walitiwa ndani kwa muda katika mji wa Nishni- Novgorov nchini Urusi.
Wanaharakati hao kutoka nchi za nje walikuwa wanakusudia kushiriki katika mkutano wa hadhara ili kumkumbuka mwandishi habari wa kirusi , Anna Politkovskaya alieuawa kwa kupigwa risasi mjini Moscow mwaka moja uliopita. Mwandishi huyo alikuwa mkosoaji mkali wa serikali.
Shirika la haki za binadamu-Human Rights First limesema kuwa watu hao walikamatwa kwa madai kwamba walikiuka taratibu za viza.