MORONI:Wanajeshi watiifu wakidhibiti kisiwa cha Nzuwani | Habari za Ulimwengu | DW | 03.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MORONI:Wanajeshi watiifu wakidhibiti kisiwa cha Nzuwani

Wanajeshi watiifu kwa rais wa kisiwa cha umoja wa Komoro cha Nzuwani leo wameudhibiti mji mkuu wa Mutsamudu.

Hayo yametokea baada ya kukataa kujiuzulu kwa rais wa Nzuwani kanali Mohamed Bakari ambae ametangaza nia yake ya kutaka kugombea katika uchaguzi wa marais wa visiwa wa mwezi ujao.

Hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa kwamba huenda kutatokea mapinduzi kwa mara nyingine tena katika nchi ambayo imekumbwa na mapinduzi na majaribio ya kujitenga kwa kipindi cha miaka 30.

Waziri wa habari Madi Ali ametoa taarifa kupitia radio ya Komoro.

Taarifa hiyo imelaani hatua ya kukiteka kisiwa cha Anzuwani na ameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com