Mkutano wa kilele kuhusu hatima ya nishati ya Diesel
2 Agosti 2017Mazungumzo baina ya wanasiasa wa Ujerumani na watengenezaji wa magari bado yanaendelea leo, hata baada ya chama cha wenye viwanda vya magari VDA kusema , wamekubali kupunguza utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira kwa kuboresha programu maalum katika magari ya dizeli milioni 5.
Duru zilizoko karibu na majadiliano hayo zimesema mazungumzo hayo baina ya mawaziri kadhaa, mawaziri wakuu wa majimbo na wakuu wa viwanda vya magari bado yanaendelea na yamegawanywa katika makundi kadhaa.
Hapo mapema leo, chama cha wenye viwanda vya magari VDA kimesema kitaweka program mpya ya uedneshaji ingini katika magari milioni 5 ili kufanya mfumo wa kuchuja moshi uweze kufanyakazi vizuri zaidi na kushusha utoaji wa gesi zinazochafua mazingira kwa asilimia 25 hadi 30 katika magari hayo.