1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Misri na Uturuki zakubaliana kuboresha uhusiano

30 Mei 2023

Viongozi wa Misri na Uturuki wamekubaliana kuboresha uhusiano wa kidiplomasia, ushirikiano na kubadilishana mabalozi ikiwa ishara mpya ya kustawishwa kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya muongo mmoja wa uhasama.

https://p.dw.com/p/4RyDf
WM in Katar 2022 | Treffen Recep Tayyip Erdogan und Abdulfettah al-Sisi
Picha: DHA

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa ofisi ya rais wa Misri, Rais Abdel-Fattah al-Sissi alimpigia simu mwenziwe Recep Tayyip Erdogan na kumpongeza kuchaguliwa tena kuwa rais wa Uturuki.

Soma pia: Misri imeahidi "mshikamano na huruma" kwa Syria

Uhusiano kati ya Misri na Uturuki ulidorora katikati ya mwaka 2013 baada ya jeshi likiongozwa na al-Sissi, kumpindua rais wa Misri kwa wakati huo Mohammed Morsi.