1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Miji miwili ya Ukraine yashambuliwa na makombora ya Urusi

2 Januari 2024

Miji miwili mikubwa ya Ukraine ilishambuliwa vikali kwa makombora ya Urusi usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa taarifa ya gavana wa jimbo la Kharkiv, mtu mmoja ameuawa na wengine wapatao 41 wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4an7V
Ukraine | Urusi
Maafisa wa zima moto wakifanya kazi ya kuzima moto katika jengo lililoharibiwa baada ya shambulio la Urusi huko Kyiv, Ukraine.Picha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

Miji miwili mikubwa ya Ukraine ilishambuliwa vikali kwa makombora ya Urusi usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa taarifa ya gavana wa jimbo la Kharkiv,  mtu mmoja ameuawa na wengine wapatao 41 wamejeruhiwa.

Wakati huo huo, katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, meya Vitali Klitschko amesema takriban watu12 wamejeruhiwa. Urusi imeongeza mashambulio nchini Ukraine mnamo siku za karibuni na kufikia kiwango kikubwa kabisa tangu kuanza kwa vita baada ya kuilaumu Ukraine kwa kuushambulia mji wake wa mpakani wa Bolgorod na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Soma kuhusu: Putin ataja shambulizi katika mji wa Belgord kuwa ''tukio la kigaidi''

Urusi imesema inalenga miundombinu ya kijeshi nchini Ukraine lakini serikali ya Ukraine imeripoti vifo vya raia kutokana na mashambulizi hayo ya Urusi ya kila siku. Rais wa Ukraine, Volodmyr Zelensky amelaani mashambulizi haoy ya Urusi.