Mataifa kadhaa duniani yasherehekea Eid al-fitr 2026
20 Machi 2026
Waislamu walikusanyika katika Msikiti Mkuu wa Makka kusali, salaya Eid kuashiria mwisho wa Ramadhani.
Vilevile Sala ya Eid imefanyika na sherehe zinafanyika katika maeneo mbalimbali dunaini ingawa katika nchi zingine sikuu hii itasherehekewa hapo kesho Jumamosi, Eid kwa kawaida hupokelewa kwa furaha na msisimko na huadhimishwa na sala na sherehe zinazojumuisha mikusanyiko ya kifamilia, watu kutembeleana na kuvaa nguo mpya. Hata hivyo mwaka huu sikukuu ya Eid pia inaadhimishwa na vita vinavyoendelea nchini Iran na katika sehemu nyingi za Mashariki ya Kati.
Milipuko mikubwa imetikisa mji wa Dubai huku mifumo ya ulinzi wa anga ikizuia mashambulizi yaliyoulenga mji huo mapema leo wakati watu walipokuwa wanasali sala Eid al-Fitr.
Wakazi wa Gaza wanajitahidi kukidhi mahitaji ya Eid al-Fitr, hata katika kiwango cha msingi, licha ya hali mbaya ya maisha kutokana na vita katika eneo hilo na kupungua kwa mapato ya raia.
Masoko maarufu yalishuhudia wimbi la watu asubuhi ya leo wakinunua mahitaji kwa ajili ya Eid, katika juhudi za kuleta furaha majumbani mwao na kwa watoto wao baada ya kushindwa kusherehekea katika kipindi chote cha vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza.
Katika Falme ya Kiarabu, sala za nje kwa ajili ya Eid zimepigwa marufuku ni lazima zifanyike ndani ya misikiti kwa sababu za kiusalama. Nchini Kuwait, mamlaka zimepiga marufuku kwa muda matamasha, na sherehe za harusi wakati wa Eid al-Fitr ili kupunguza mikusanyiko mikubwa ya watu.
Wakati huo huo Pakistan na Afghanistan zimetangaza kusitishwa kwa mapigano wakati wa sherehe ya Eid, baada ya mapigano mabaya kati ya nchi hizo mbili ambayo yamesababisha vifo vya ya watu mapema wiki hii.