1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
DR Kongo Kinshasa City
Picha: Ute Grabowsky/photothek/imago images

DRC washerehekea sikukuu ya Eid al-Fitr

Mitima Delachance
2 Mei 2022

Waislamu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamesherehekea siku kuu ya Idd el-Fitr baada ya kuhitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani leo jumatatu.

https://p.dw.com/p/4Ajjm

Hafla  zilifanyika katika mikoa mbali mbali ya nchi hiyo. Katika mkoa wa Kivu kusini, waislamu wanaeleza kwamba haikuwa rahisi kutokana na athari za kiuchumi. Waislamu mjini Bukavu wamefanya swala ya  Idd el-Fitr katika  kiwanja cha michezo ya soka kinachoitwa "La Concorde” katika mtaa wa Kadutu, huku wengine wakifurika ndani ya msikiti mkuu wa Bukavu eneo la Nyawera mtaani Ibanda. Aisha Ibrahim ni miongoni mwao, anaeleza namna mwezi wa Ramadhani ulivyokuwa.

Kando ya msikiti wa Nyawera, Juma Kashera, muislamu mwenye umri wa miaka ipatayo thelathini anasema  kwamba Ramadhan mwaka huu haikuwa rahisi kutokana na hali ya kupanda bei ya vyakula muhimu, na kuongeza kuwa ili kuimudu hali hiyo, Waislamu walikuwa na mshikamano.

Uganda Islam l Eid al-Fitr l Zuckerfest
Waumini wa Kiislamu nchini UgandaPicha: Lubega Emmanuel /DW

Pamoja na kutoa ujumbe wa amani na mapendo kati ya waislamu na watu wote, katibu wa jumuiya ya waislamu wa Congo katika mkoa wa kivu kusini Cheikh Mahmoudu Murhimanya Bashimbe amekumbushia ombi la wasilamu wa Congo la kuitaka serikali itambuwe rasmi siku za sherehe za waislamu kwa kuzitangaza kuwa siku za mapumziko.

Pamoja na kuhitimisha  mwezi mtukufu wa ramadhani, baadhi ya waislamu wameahidi kufanya mafungo mengine ya siku sita za mwezi wa Shawal kuanzia kesho.