Mashambulizi ya Urusi yauwa watu 16 Ukraine
17 Aprili 2026
Ukraine inasema mashambulizi hayoya anga ndiyo mabaya zaidi kuwahi kufanywa nchini humo katika kipindi cha wiki kadhaa.
Karibu droni 700 na dazeni kadhaa za makombora yalitumika katika mashambulizi hayo. Maafisa wa Ukraine wanakiri kuwa hifadhi zao za mifumo ya kujilinda zinaelekea kuisha.
Haya yanafanyika wakati ambapo Umoja wa Ulaya unatazamiakuanza kuipa Ukraine mkopo wa yuro bilioni 90 katika robo ya pili ya mwaka.
Haya ni kwa mujibu wa kamishena wa uchumi wa Umoja wa Ulaya Vladis Dombrovskis aliyeyasema hayo katika mazungumzo na shirika la habari la Ufaransa AFP.
Dombrovskis anasema kushindwa kwa Viktor orban katika uchaguzi wa Hungary kunawapelekea sasa kuwa katika nafasi ya kuweza kuutoa mkopo huo kwani Orban pekee ndiye aliyekuwa kikwazo.