1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya droni yawauwa watu wawili Ukraine

18 Januari 2026

Watu wawili wameuawa baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya droni nchini Ukraine usiku wa kuamkia Jumapili. Makumi ya watu wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/570Vn
Kyiv, Ukraine 2026
Juhudi za kuzima moto zikiendelea katika moja ya maeneo ya Ukraine baada ya shambulio ya droni la UrusiPicha: Thomas Peter/REUTERS

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi hayo yamehusisha zaidi ya droni 200. Zelensky kupitia ukurasa wake wa jukwaa la X ameongeza kuwa maeneo yaliyolengwa na Urusi ni pamoja na Kharkiv, Dnipro, Zaporizhzhia, Khmelnytskyi, na Odesa

Zaidi ya watu 200,000 hawana umeme Zaporizhzhia

Wakati huohuo Gavana wa eneo la  Zaporizhzhia la Ukraine linalodhibitiwa na Urusi kwa aslilimia 75 Yevgeny Balitsky amesema zaidi ya watu 200,000 hawana umeme baada ya mashambulizi ya droni yaliyofanywa na Ukraine jana Jumamosi.