1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya Urusi yawauwa watu saba Ukraine

8 Machi 2026

Watu wasiopungua saba wameuwawa nchini Ukraine, baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya droni na makombora usiku wa kuamkia Jumamosi 07.03.2026. Miongoni mwa waliouwawa ni wanawake na watoto.

https://p.dw.com/p/59yJ8
Ukraine Kharkiv 2026 | Jengo lililoathiriwa na mashambulizi ya Urusi
Juhudi za kuzima moto na uokoaji mjini Kharkiv, Ukraine baada ya mashambulizi ya UrusiPicha: Vyacheslav Madiyevskyy/REUTERS

Mamlaka za Kyiv zimesema miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni mashariki mwa mkoa wa Kharkiv bambapo ghorofa inayotumika kama makazi ya watu iliangukiwa na kombora.

Miundombinu ya nishati na reli yalengwa

Akiyazungumzia mashambulizi hayo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameeleza kuwa mashambulizi hayo ya Urusi yalihusisha droni zipatazo 480 na makombora 29 yaliyolenga sekta ya nishati na miundombinu ya reli katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Sehemu ya bandari katika mkoa wa Odesa ililengwa pia hali iliyosababisha makontena yaliyokuwa na mafuta kushika moto na kuteketeza ghala la nafaka.