Marekani yatatiza juhudi za WHO za kupata kiongozi | Matukio ya Afrika | DW | 29.10.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Marekani yatatiza juhudi za WHO za kupata kiongozi

Mchakato wa Shirika la Biashara Duniani WTO wa kuchagua kiongozi mpya umekwama baada ya Marekani kumkataa mwanamke wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala aliyependekezwa kama mkurugenzi mkuu wa shirika hilo.

Utawala wa Rais Donald Trump tayari umeshadhoofisha uwezo wa shirika hilo la WTO kama msuluhishi wa masuala ya kibiashara ulimwenguni kwa kuzuia teuzi za jopo lake la rufaa. Na sasa linatishia kukwamisha uteuzi wa uongozi wa shirika hilo kwa wiki au miezi kadhaa ijayo. Shirika hilo la WTO limeitisha mkutano mnamo Novemba 9, ambapo linatarajia litakuwa limeshapata uungwaji mkono wa kutosha wa kuteuliwa mgombea huyo kutoka Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala.