Mapigano yasababisha umwagaji damu kusini mwa Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 19.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mapigano yasababisha umwagaji damu kusini mwa Irak

BAGHDAD: Si chini ya watu 70 wameuawa katika mapigano yaliyozuka nchini Irak kati ya wanajeshi na kundi la watu wa madhehebu ya Kishia.Polisi leo hii wamesema,hadi waumini 35 wa kundi fulani la kidini la Kishia,waliuawa katika mji wa Basra kusini mwa nchi na 18 wengine mjini Nasiriyah kama kilomita 350 kusini mwa mji mkuu Baghdad. Polisi na raia wa kawaida pia waliuawa katika mapambano hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com