Maoni: 2016 mwaka wa kutisha kwa mara nyingine
27 Desemba 2016Mwaka 2016 pia ulikuwa mwaka wa kutisha. Dunia imetumbukia katika hali ya mparaganyiko. Katika mashariki ya kati vita vinaendelea - nchini Syria , Yemen , Libya na pia Iraq. Kundi linalojiita Dola la Kiislamu , linalofanya unyama wa kuogofya, mauaji, ugaidi wa itikadi kali, bado haujamalizwa. Hali tete ya vuguvugu la mapinduzi ya mataifa ya kiarabu ndiyo yaliyozusha hali hii , kupitia ukandamizaji , matumizi ya mabavu, na udikteta. Na kutokana na athari hizo na kitovu cha tetemeko hilo kutoka katika eneo hilo, huenda ikatikisa siasa za dunia pamoja na kuzusha mripuko wa kijamii, ama hata pengine tayari umezusha hali hiyo.
Inaonekana kwamba eneo hilo la mashariki ya kati limetumbukia katika vita miaka 30 iliyopita, ambapo koo, kabila na jamii za kidini ni mambo ambayo yanasababisha mapambano.
Katika pwani za mataifa ya bara lote la Ulaya waliwasili wakimbizi kutoka mataifa ya Mashariki ya Kati na kusababisha mshituko na mtikisiko. Mzozo wa wakimbizi tayari umeweka wazi, kwamba suala la "mshikamano wa mataifa ya Ulaya " ni neno ambalo limeingia kiwingu .
Brexit , neno linalotumika kwa kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya , limeiingiza jamii ya Ulaya katika mashaka makubwa. Kazi ya pamoja ya kutafuta amani iliingia majaribuni , na jamii ilielekeza njia ya kuchukua katika mustakabali wa nchi yao.
Kwa sasa ni hakika , kwamba pamoja na Ulaya Mashariki kurejea katika hali ya mataifa kujiamulia mambo yao wenyewe na kuwa na utambulisho wake, katika miaka ijayo pia mataifa ya Ulaya Magharibi yanaonekana kuwa yatabadilisha utendaji wa madaraka. Nchini Uholanzi inaonekana kupitia Geert Wilders na nchini Ufaransa pia bila shaka kutakuwa na rais mpya , huenda ni Mkatoliki, "mfuasi wa siasa za Thacher", ni mapinduzi ya aina gani yatakayotokea.
Na hata nchini Ujerumani , nchi ambayo ilionekana kuwa mhimili wa uthabiti , kutakuwa na uchaguzi mwezi Septemba. Hakuna mtu kwa hivi sasa anayeweza kufikiria , kwamba Angela Merkel, atakuwa na muungano gani , ama kwamba atabaki katika wadhifa wa Ukansela.
Ni ngome kuu ya siasa za ndani na nje duniani , na hii ni kwa miaka takriban 11 iliyopita. Lakini hata hapa nchini chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Altenative for Germany AfD, kimeingia katika bunge la taifa na kinaonekana kupata uungwaji mkono mkubwa. Hapa Ujerumani pia watashinda wale wenye mawazo ya siasa kali za mrengo wa kulia, hata kama hawataweza kuchukua madaraka ya nchi.
Ujerumani itaendelea kuwa na uongozi imara. Na ndio sababu Ujerumani itaendelea kuwa sehemu ya utulivu katika siasa za dunia ambazo hazina utulivu na za wasi wasi. Na hii ni licha ya shambulizi ya kigaidi la mjini Berlin muda mfupi kabla ya sikukuu ya Krismasi, shambulio ambalo liliitikisa nchi hii kwa kiasi kikubwa.
Mwandishi: Alexander Kudascheff . /ZR / Sekione Kitojo
Mhariri : Yusra Buwayhid