Manchester United ina miadi leo na FC Porto | Michezo | DW | 15.04.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Manchester United ina miadi leo na FC Porto

Arsenal iko nyumbani kumenyana na Vilarreal ya Spian.

default

Wayne Rooney ashangiria bao lake.

Ni mwezi tu uliopita ilipobainika kuwa mabingwa wa dunia Manchester united ni beberu nunda lisiloshindika. Lakini wamewasili Porto leo huku ndoto yao ya kuvaa mataji 5 msimu huu ikijikuta mashakani.

Manu imetamba kwa kutwaa Kombe la dunia na Carling Cup na hakuoneshi kuna shaka shaka kuwa itatamba katika premier League nyumbani msimu huu,halafu Kombe la FA.Lakini Kombe wanalolitamani sana ni hili la leo champion League.Wareno wa FC Porto wameandaa mtego wa kuwanasa M anu na ikiwa hawatachunga ,watavuliwa taji usiku wa leo kama mabingwa wenzao wa zamani Bayern munich hapo jana.Kutoka sare 2:2 na Porto tena nyumbani,yalikuwa madhambi makubwa kwa Manu na ikiwa jogoo lao la Ureno, Cristiano Ronaldo halitawika leo,basi buriyani Manu alao msimu huu.

Manchester united ikionekana ina ufa katika ngome yake hivi karibuni na shak shaka nyingi ziko kwa beki-mshahara Rio Ferdinand ambae bado anaugua -maumivu ambayo yalimkosesha duru ya kwanza ya kinyanganyiro hiki.Mshambulizi kutoka Bulgaria Dimitry Berbatov anachechemea na hii yaweza kumfanya kocha Sir Alex Ferguson kumwita tena chipukizi wa miaka 17 Federico Macheda kuliokoa jahazi la Manchster United lisizame leo huko Porto.

Porto inatamba wakati huu na Jumamosi iliikomea Estrela Amadora mabao 3-0 ili kubakisha uongozi wao wa pointi 4 kileleni mwa ligi ya Ureno. FC Porto chini ya kocha Jose Mourinho,walikiwisha litwaa Kombe hili na mwaka huu wanadai wanalitaka tena.

Shida lakini iko kwa kocha wao Jesualdo Ferreira ambae ni mwiko leo hata kunyemelea chaki ya uwanja kuwapa mawaidha.Watabidi kujitegemea wenyewe.Sitapenda kuagua matokeo ya mpambano huu.

Ama ndugu zao Manu-Arsenal kibarua chao si kigumu sana kama cha Manu.Wao wanatamba leo nyumbani na jogoo lao mtogo Emmanuel Adebayo, aliewapatia lile bao walipotoka suluhu na Vilarreal wiki iliopita amejinoa barabara. Likitia bao jengine leo,litawathibitishia waspain kwanini amechaguliwa "mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika".

Muandishi : Ramadhan Ali

Mhariri: M.Abdul-Rahman

 • Tarehe 15.04.2009
 • Mwandishi Munira Muhammad
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HXei
 • Tarehe 15.04.2009
 • Mwandishi Munira Muhammad
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HXei
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com