1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

FC Ingolstadt

Ingolstadt ndiyo klabu changa kabisaa katika Bundesliga, ikiundwa mwaka 2004 baada ya kuungana ESV Ingolstadt na MTV Ingolstadt. Waliingia Bundesliga kwa mara ya kwanza 2015 baada ya kushinda ligi ya daraja la pili.

Katika mji ulio na mgawiko dhahiri wa kisoka, Peter Jackwerth aliziunganisha klabu mbili kubwa kabisaa za mji huo na kuunda FC Ingolstadt 04. Ikianzia katika ligi la daraja la nne ya kikanda, klabu hiyo ya Bavaria ilipanda kwa kasi na kufika ligi ya daraja la pili ya Bundesliga miaka sita tu baada ya kuungana. Ikicheza katika uwanja wa Audi-Sportpark, Ingolstadt bado ina kibarua cha kujidhihirisha kama klabu ya daraja la juu. Kwa habari zote kuhusu Ingolstadt, usitazame mbali ya ukurasa huu.