Mahojiano ya DW na Cem Özdemir | Uchaguzi wa Ujerumani 2017 | DW | 25.07.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Uchaguzi mkuu Ujerumani

Mahojiano ya DW na Cem Özdemir

Mgombea wa chama cha Kijani nchini Ujerumani Cem Özdemir ametoa lawama kali dhidi ya Uturuki katika mahojiano aliyofanyiwa na DW anasema Ujerumani inapaswa kuangalia upya sera zake juu ya Uturuki.

Katika mahojiano hayo na DW mgombea huyo wa chama cha Kijani Cem Özdemir alisema Ujerumani inapaswa kuangalia upya sera zake juu ya Uturuki ambapo mwanasiasa huyo kwa ujumla anazilaumu sera za kansela Angela Merkel juu ya Uturuki tangu bibi Merkel alipoingia madarakani mnamo mwaka 2005.

Kabla ya hapo serikali ya mseto ya vyama vya Social Demoktarik SPD na Chama cha Kijani ilikuwa inawaunga mkono wale waliokuwa wanatetea mageuzi nchini Uturuki. Lakini baada ya kansela Merkel kusisitiza wazo la kuipa hadhi Uturuki katika mchakato wa kujiunga na Umoja wa Ulaya hapo ndipo aliposababisha kuvunjika kwa watetezi wa mageuzi nchini Uturuki.  Cem Özdemir katika mahojiano hayo alisisitiza kuwa juhudi zozote za kujaribu kujenga "jumuiya inayofanana nchini Ujerumani" lazima zipingwe mara moja.AlisemaErdogan anataka kujengaUturuki ndani ya Ujerumani kwa hilo naweza alisema wazi kwamba halitawezekaalionya pia kwamba katika siku za usoni hakuna tena kupokea fedha kutoka Uturuki kwa ajili ya misikiti hapa Ujerumani. 

Özdemir Alitoa mfano wa wafuasi wengi wa upinzani raia wa Uturuki ambao wamekuja kwake na kueleza wasiwasi juu ya usalama wao hapa nchini Ujerumani. Juu ya swala la Urusi kuwekewa vikwazo mgombea huyo wa chama cha Kijani Cem Özdemir wala hakutafuna maneno alipoulizwa swali hilo na mhariri mkuu wa DW Ines Pohl. Alisema haoni sababu kwa nini Urusi isiongezewe vikwazo vikali.

Kuanzia kushoto Jaafar Abdul-Karim, Cem Özdemir, Mhariri mkuu wa DW Ines Pohl (DW/R. Oberhammer)

Kuanzia kushoto Jaafar Abdul-Karim, Cem Özdemir, Mhariri mkuu wa DW Ines Pohl

Özdemir katika mahojiano hayo ambayo yaliangazia zaidi sera za Ujerumani za mambo ya nje alisisitiza kwamba Urusi ni lazima iwekewe vikwazo zaidi kwa kujiingiza kwake nchini Ukraine.

Mazingira ni mada muhimu kwa Özdemir

Vilevile mahojiano hayo yaligusia maswala ya mabadililiko ya hali ya hewa ambapo huenda chama cha Kijani pamoja na chama cha Waliberali cha FDP vinaweza kushiriki katika kuunda serikali ya mseto na chama kinachoongozwa na kansela Angela Merkel baada ya kumalizika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo tarehe 24 mwezi Septemba. Je ni kipi cha ajabu kitakacholetwa na chama hiki cha Kijani katika serikali ya mseto wa aina hii?  Jibu la Özdemir lilikuwa ni kuilaumu serikali ya kansela Angela Merkel alisema ''Kwa bahati mbaya Ujerumani haishiki nafasi ya mwanzo linapokuja swala la kulinda mazingira.  Mgombea huyo wa chama cha Kijani anasema inawezekana kansela Merkel akaonyeshwa kama bingwa wa dunia katika vichwa vya habari, akilinganishwa na rais wa Marekani Donald Trump yeye ni anaibuka kama "mwanga mkali," lakini ukichimba chini zaidi unakuta mara nyingi sera zake si chochote si lolote katika ulimwengu huu''.

Özdemir anasisitiza kwamba anaamini "Ujerumani inaweza kufanya vizuri zaidi." Anasema inapaswa kuwepo na msimamo thabiti kati ya mazingira na uchumi.  Akiwa sasa ana umri wa miaka 51 Özdemir alikuwa ni mjiongoni mwa watoto wa wahamiaji aliyelazimika kwenda kwenye shule zilizotengwa kwa ajili ya watoto wahamiaji katika miaka ya 70 na siku moja mwalimu alipowauliza ni nani kati yao aliyetaka kujiunga na shule ya upili Özdemir aliinua mkono lakini anakumbuka jinsi alivyogeuka kuwa kituko darasani mwake.

Özdemir aliruka kiunzi hicho hasa pale alipodhaniwa kuwa hataweza.  Mfano mwingine ni mwaka 1994 pale alipoibuka kuwa mbunge wa kwanza nchini Ujerumani mtoto wa wahamiaji aliyeingia bungeni kukiwakilisha chama chake cha Kijani.

Mwandishi: Zainab Aziz/Scholz, Kay-Alexander/LINK: http://www.dw.com/a-39747670

Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com