1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Trump na Putin wawindana Syria

Sekione Kitojo
12 Aprili 2018

Wahariri wa magazeti  ya  Ujerumani wameangalia  masuala  ya mzozo unaoendelea  kujitokeza nchini  Syria  kati ya Urusi  na Marekani, kuhojiwa kwa  mkuu  wa mtandao wa kijamii  wa Facebook Mark Zuckerberg.

https://p.dw.com/p/2vuz4
President Trump comments on Syria, FBI raid of Michael Cohen's office at White House
Picha: picture alliance / Newscom

Tukianza  na  gazeti  la  Der tagesspiegel la  mjini  Berlin linaandika kuhusu  mvutano unaoelekea  katika  mashambulizi  ya muungano unaoongozwa  na  Marekani dhidi  ya  vituo vinavyotengeneza  gesi ya  sumu  nchini Syria. Mhariri  anaandika  kwamba  Trump anamtwika  dhamana dikteta  wa  Syria Bashar al-Assad kwa shambulio la  gesi  ya  sumu katika  eneo lililokuwa  linadhibitiwa  na waasi  la  Douma. Mhariri  anaendelea:

Syria  pamoja  na  Urusi inayoitetea  nchi  hiyo  zote zinapinga madai hayo, zikisema  ni suala  lililopangwa. Israel imekuwa  ikifuatilia maeneo  ambayo majeshi  ya  Iran yapo na  Iran imetangaza kulipiza kisasi iwapo yatashambuliwa. Raia wa  mataifa  ya  magharibi wanapaswa kudai kuwapo uwazi wa kutosha  kutoka  katika  serikali zao  kuhusiana  na  suala  hili. Ushahidi  kuhusiana  na  ufahamu  wa mashirika  ya kijasusi  kuhusu  tukio  hilo hadi  sasa  haupo. Kuna sababu  nzuri , Putin kama  mtu  hatari  pamoja  na  Trump kuwazuwia , na  kuyaamini  mashirika  ya  kutetea haki  za binadamu, badala ya  kuunga mkono Israel  katika mapambano  dhidi ya  utawala  wa  Assad na viongozi  wa  kidini  wa  Iran.

Syrien Mutmaßlicher Giftgasangriff in Duma
Waathirika wa shambulio la sumu linalofikiriwa lilifanywa na serikali ya Syria wakipatiwa matibabuPicha: Reuters/White Helmets

Nae mhariri  wa  gazeti  la Westfälische Nachrichten  la  mjini Münster  kuhusiana  na  mada  hiyo  anaandika, kwamba aina  hii  ya matamshi  ya  kivita yanakwenda  mbali  sana , kuliko  ilivyokuwa hapo  awali. Mhariri  anaandika:

Hali  ni mbaya  kuliko ilivyokuwa. Trump  anataka  kulipiza  kisasi, Putin  anapinga. Ni vita  vya  maneno  baina  ya  mataifa  mawili yenye  nguvu. Mpaka  wa  kuwa  na  burasa  na  majadiliano  kwa pande  zote  mbili, umevukwa.

Wengi miongoni  mwa  watumiaji  bilioni  mbili  wa  mtandao  wa kijamii  wa  facebook wenyewe wanamakosa. Anaandika  mhariri  wa gazeti  la  Der neue Tag la  mjini  Weiden  kuhusiana  na  hatua  ya kamati  ya  baraza  la  seneti  nchini  Marekani  kumuita  kwa mahojiano  mkuu  wa  mtandao  huo Mark Zuckerberg. Mhariri anaadika.

Wachache  wanatambua  kile  walichokiweka  na kukiacha katika mtandao  huo. Kwasababu  wengi  hawaangalii  matumizi  yao  ya msingi  ya  mtandao  wa Facebook, ili kuzuwia  ukusanyaji  wa  data unaofanywa na  mtandao  huo, ingekuwa somo  kubwa  kwa  shirika hilo  linalojitangaza  kwamba  lina nia  njema  na  watumiaji wake kutoka  Menlo Park. Na  nani  anajua , huenda  mtandao  huo  wa kijamii  ukapotea  haraka  kama  ulivyojitokeza. Halafu kutajitokeza kitu  kingine kikubwa  katika  ulimwengu  wa  digitali.

Mhariri  wa  gazeti la General-Anzeiger  la  mjini  Bonn  anazungumzia kuhusu  mkutano  wa  kufahamiana  miongoni  mwa  mawaziri wanaounda  serikali  ya  mseto  inayoongozwa  na  kansela  Angela Merkel  wa  Ujerumani. Mhariri  anaandika:

Nia  ya  kutaka  kupata msimamo  wa  pamoja  ilikuwapo,  hali ya msisimko ilikuwa  nzuri, alisema  kansela  Angela  Merkel  na makamu  wake  Olaf Scholz. Lakini haitoshi , haitoshi  kabisa. Anaandika  mhariri, kwa  sababu  hilo  ni  jambo  la  kawaida  kwa serikali  yenye  uchumi  mkubwa  kabisa  barani  Ulaya, ili kulinda heshima  ya  kisiasa  na  kiuchumi  ya  nchi  hii muhimu barani Ulaya. Serikali  ambayo  inatakiwa  kuamua  ina  msimamo  gani  katika mzozo  wa  Syria, na  jinsi  gani  itashughulikia  vita  vya  kibiashara duniani. Na  haitoshi, wakati waziri  wa  fedha  Scholz  akisema, kwamba kila kitu kitawezekana  tu  kwa  kuwa  na  sera  imara  za bajeti. Hii  ni  kweli  takriban iwapo hazina imejaa, uchumi  unakua kwa kasi  na uongozi  unafanya  vizuri.

 

Mwandishi:   Sekione  Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Iddi Ssessanga