Loew ana kazi kubwa ya kukifanyia kikosi cha Ujerumani | Michezo | DW | 12.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Loew ana kazi kubwa ya kukifanyia kikosi cha Ujerumani

Ujerumani imefuzu katika dimba la UEFA Euro 2016 kwa kumaliza kileleni mwa kundi D lakini namna ilivyopata ushindi wake wa magoli mawili kwa moja katika mchuano wake wa mwisho dhidi ya Georgia inawacha maswali

Ujerumani ilihitaji pointi moja tu katika mchuano wa jana mjini Leipzig ili kujikatia tikiti ya kwenda Ufaransa lakini ikalazimika kuwa na dakika 90 za hofu kubwa dhidi ya Georgia. Na Reus siyo mchezaji pekee aliyekosa kutamba mbele ya lango kwa sababu Thomas Mueller na Mesut Oezil pia walipoteza nafasi nzuri za wazi.

Akizungumza baada ya mechi hiyo kocha Joachim Loew alisema Reus ni mchezaji mzuri sana asiyestahili kutupa nafasi kama alizopata. Loew amesema wazi kuwa analenga kuufanyia mabadiliko mfumo wa mchezo wa kikosi cha taifa ili kuhakikisha kuwa wanaumiliki vyema mpira.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga