1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen waazimia kunyanyua mataji matatu msimu huu

3 Aprili 2024

Viongozi wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Bayer Leverkusen leo wanaingia uwanjani kwao Bay Arena kuialika timu ya daraja la pili Fortuna Düsseldorf katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho DFB Pokal.

https://p.dw.com/p/4eOmp
 Bayer Leverkusen
Kikosi cha Bayer LeverkusenPicha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Viongozi wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Bayer Leverkusen leo wanaingia uwanjani kwao Bay Arena kuialika timu ya daraja la pili Fortuna Düsseldorf katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho DFB Pokal.

Leverkusen ambao wanapigiwa upatu kutinga fainali wako mbioni kuwania mataji matatu msimu huu, ligi kuu, kombe la shirikisho na ligi ya Ulaya ambayo tayari wameshafuzu nusu fainali, ambapo watacheza na West Ham United ya nchini England. Soma: Florian Wirtz haondoki Leverkusen msimu ujao

Klabu hiyo ambayo imekwenda mechi 39 bila kufungwa katika mashindano yote msimu huu, itapambana na FC Kaiserslautern kwenye fainali iwapo itaibwaga Düsseldorf.

Kaiserslautern walikuwa washindi wa 2-0 walipocheza na Saarbrücken hapo jana katika nusu fainali ya kwanza.