1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kusuka au kunyoa wagombea ubunge na uwakilishi CCM

Admin.WagnerD20 Agosti 2020

Halmashauri Kuu ya Chama tawala nchini Tanzania CCM, imeanza vikao vya kuteua majina ya wagombea ubunge ambao watapeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.

https://p.dw.com/p/3hEYS
Tansania Wahlen 2020 | John Magufuli
Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi John Magufuli Picha: picture-alliance/AP Photo

Majira ya saa tatu asubuhi mwenyekiti wa chama hicho na rais wa Tanzania John Magufuli amefungua mkutano huo ukiwa na akidi ya wajumbe mia moja kumi na tatu ambayo inatoa uhalali wa maamuzi yatakayoafikiwa kwa mujibu wa katiba wa chama hicho.

Akitoa maelezo mafupi kabla ya kuanza mkutano wa ndani ukiwa na dhima ya kuchaguza majina ya makada wa chama hicho watakaopeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, rais Magufuli amesema, wametumia upembuzi yakinifu kwa kupata taarifa za wagombea kutoka vyanzo mbalimbali, ili kupata mwakilishi ambae atafaa kwa taifa na chama kwa ujumla wake.

Amesema uchambuzi huo wa taarifa za wagombea umefanyika kwa kuwa miongoni mwa wagombea hao watakaopitishwa na halmashauri kuu ya chama hicho, ndio watakapochaguliwa waziri mkuu wa Tanzania, makamu wa pilli wa Rais Zanzibar pamoja na spika wa bunge.

Uteuzi kutumia vigezo vikali 

Tansania Wahlen 2020
Picha: picture-alliance/AP Photo

Aidha mwenyekiti huyo wa chama hicho kilichodumu mamlakani zaidi ya miongo minne amewataka wajumbe wa halmashauri kuu kuhakikisha wanateua mtu kulingana na sifa zake na kuweka kando, ukabila, ukanda na udini badala yake waweke mbele maslahi ya taifa na chama chao kuwakilishwa vizuri katika serikali ijayo endapo watapata ridhaa ya wapiga kura.

 

Makada wa chama hicho waliojitokeza kuomba nafasi mbalimbali za kukiwakilisha chama katika uchaguzi mkuu ni 43461 kati yao wabunge katika majimbo na viti maalum ni 10367,wawakilishi kutoka upande wa zanzibar ni 786 huku nafasi za udiwani wakijitokeza watu 33094, miongoni mwao wakiwepo kundi la vijana, wafanyakazi, wakulima na hata wawakilishi wa mashirika yasio ya kiserikali.

Awali katibu mkuu wa chama hicho Dokta Bashiru Ally alisema kutokana na ratiba za uteuzi katika tume ya taifa ya uchaguzi NEC na ile ya Zanzibar ZEC mkutano huo hautafanya uteuzi wa wawakilishi, huku baadhi ya wajumbe katika halmshauri kuu wakishindwa kuhudhuria kutokana na kuwa miongonnii mwa wagombea wa nafasi za ubunge.

Hapo baadae halmashauri hiyo inatarajiwa kupitisha majina baada ya kukamilisha zoezi hilo muhimu kwa mujibu wa chama hicho

Mwandisjhi: Hawa Bihoga DW Dodoma

Mhariri: Iddi Ssessanga