Kudorora kwa matokeo kwapandisha joto la Wakenya | Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2013 | DW | 08.03.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2013

Kudorora kwa matokeo kwapandisha joto la Wakenya

Huku Wakenya wakiendelea kusubiri kwa hamu kubwa matokeo ya urais tangu wapige kura siku ya Jumatatu, wasiwasi mkubwa uliojitokeza ni jinsi matokeo hayo yanavyotolewa kwa mwendo wa kinyonga.

Überschrift: Vote counting in Kenyan elections (PIC 2.JPG) Schlagworte: Kenyan elections 2013, Wer hat das Bild gemacht: James Shimanyula Wann und wo wurde es aufgenommen: Nairobi, Kenya, 06.03.2013 Was ist darauf zu sehen : Top officials of Kenya's Jubilee Coalition, led by Uhuru Kenyatta addressing a Press Confrere in Nairobi. from Left Charity Ngilu, Amina Abdallah, and Mutava Musyimi. James Shimanulya ist DW Korrespondent.

Kenia Wahlen

Kundi la kijamii la Concerned Kenyans Initiative limetoa wito kwa Tume ya Huru ya uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutangaa matokeo hayo jinsi yalivyo ili Wakenya waweze kurejea katika shughuli zao za kawaida na kumaliza hofu inayopanda kila kukicha.

Hofu hiyo iliongezwa zaidi baada ya mgombea mwenza wa muungano wa CORD, Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, hapo jana kutaka zoezi zima la ujumlishaji kura za urais lisitishwe kwa madai kuwa shughuli hiyo imekumbwa na udanganyifu mkubwa.

“Mfumo wa uwasilishaji matokeo umefeli kabisa na tuna ushahidi wa kutosha kwamba matokeo tunayoyapokea yana dosari”. Musyoka aliwaambia waandishi wa habari.

Mmoja wa maafisa wa uchaguzi nchini Kenya akiwasili na karatasi za matokeo kwenye ukumbi wa Bomas.

Mmoja wa maafisa wa uchaguzi nchini Kenya akiwasili na karatasi za matokeo kwenye ukumbi wa Bomas.

Kauli hiyo imeliweka taifa katika hali ya taharuki, kwani ilikuja siku moja tu baada ya IEBC kukiri kwamba kumekuwa na hitilafu katika mfumo wake wa kielektroniki wa kujumlisha matokeo na hivyo kurejelea mfumo wa uwasilishaji matokeo wa moja moja kupitia kwa maafisa wa usimamizi wa uchaguzi kutoka majimboni.

Lakini licha ya kulaumiwa kwa kuchelewesha matokeo ya urais, mwenyekiti wa tume hiyo, Ahmed Issack Hassan, anasema hakuna uwezekano wowote wa matokeo hayo "kuchezewa."

“Tume ingependa kuwahakikishia Wakenya kwamba kutokana na juhudi za maafisa wa uchaguzi wanazofanya kuthibitisha matokeo, hakuna nafasi ya matokeo hayo kubadilishwa na ikiwa kuna afisa yeyote atahusika na wizi wa kura, atakabiliwa na sheria yeye binafsi.”

Wakati Wakenya waliokusanyika nje ya ukumbi wa kukusanya matokeo wa Bomas jijini Nairobi wakigandisha macho yao katika ubao wa matokeo, lakini kwa muda wa masaa sita kuanzia saa 8:00 usiku, ubao huo haukutoa mabadiliko yoyote ya kura ya urais.

Jukumu sasa linaachiwa tume ya uchaguzi kuwapa matumaini Wakenya kwa kutangaza matokeo ya urais.

Mwandishi: Alfred Kiti/DW Nairobi
Mhariri: Mohammed Khelef

DW inapendekeza

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com