1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Raila Odinga

Raila Amolo Odinga, anaefahamika pia kwa wafuasi wake kama Agwambo, Tinga, Baba, RAO, na Jakom ni mwanasiasa wa nchini Kenya.

Odinga alijitupa katika ulingo wa siasa nchini Kenya mwaka 1992, alipochaguliwa kuwa mbunge wa Langata. Aliteuliwa kuwa waziri wa nishati kuanzia 2001 hadi 2002, na kisha waziri wa barabara, ujenzi na nyumba kuanzia 2003 hadi 2005. Alikuwa mgombea mkuu wa upinzani katika uchaguzi wa 2007. Kufuatia uchaguzi zilizofuatia uchaguzi huo, Odinga aliteuliwa kuwa waziri mkuu katika makubaliano ya kugawana madaraka na rais Mwai Kibaki Aprili 2008. Alishika nafasi ya pili katika uchaguzi mkuu wa 2013. Odinga ndiyo kiongozi mkuu wa muungano wa CORD, uliyoundwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2013 na ndiyo chama kikuu cha upinzani nchini Kenya.

Onesha makala zaidi