Kinyanganyiro cha madaraka Thailand | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Kinyanganyiro cha madaraka Thailand

Nini hatima ya ufalme wa Thailand ?

Wanajeshi na waandamanaji.

Wanajeshi na waandamanaji.

Wapinzani wa serikali ya Thailand, wameamua kusimamisha maandamano yao alao kwa sasa.Hatahivyo, inaonekana kana kwamba,hatima ya Thailand inaamuliwa majiani na mitaani.Sio tu hatima ya serikali iko mashakani bali pia hata kuselelea kwa Ufalme wa nchi hii.Serikali kwa kuingiwa na hofu, imetumbua macho na kuwapururia kamba waandamanaji tena kwa muda mrefu na sasa na yamkini ,muda umepita kuweza kulizima .

Damu inayomwaika katika barabara za Bangkok,vizuwizi vya majiani vinavyowaka moto,risasi zinazofyatuliwa hewani na herwa ya kutoa machozi, ndio picha zinazoonekana kutoka Bangkok.Vikosi vya ulinzi kwa taabu sana vikimudui kurejesha hali ya utulivu na nidhamu mjini humo baada ya waandamanaji kuzusha fujo na machafuko,kushambulia tangu mali ya serikali hata za kibinafsi,kuhatarisha maisha ya watu na wakati huo huo wakipaza vilio vya demokrasia.

Ni kwa muda mrefu serikali inayoongozwa na chama cha Democratic Party ,imewapururia kamba wakosdoaji wake na kukabiliana na waandamanaji barabarani kwa upole kabisa.Vikosi vya usalama hata havikuingilia kati ,pale wapinzani wakivaa fulana nyekundu walipoivamia Hoteli -kituo cha mkutano wa kilele wa Jumuiya ya nchi za kusini-mashariki mwa Asia-ASEAN huko Pattaya, ambako viongozi wa nchi 15 walikusanyika.

Pale juzi jumapili,gengi moja lilipouhujumu mlolongo wa magari wa waziri mkuu, na kuiipga gari lake pamoja na kumjerhi vibaya mtumishi wa waziri mkuu huyo,vikosi vya usalama havikujua vifanye nini bali vikitumbua macho tu.

Jeshi la Thailand lina historia isiopendeza: Kwani, tangu kuondoshwa mfumo wa ufalme kumiliki mamlaka yote nchini hapo 1932,jeshi limenyakua madaraka jumla ya mara 18.Mara ya mwisho kufanya hivyo ilikua septem ba ,2006 pale jeshi lilipomtimua madarakani waziri mkuu Thaksin Shinawatra,aliechaguliwa na wingi mkubwa wa wananchi wa Thailand.Wakati siku za nyuma wanajeshi walipata sifa mbovu kwamba hawakawii kufyatua risasi, mapindizi yao ya miaka 2 na nusu iliopita kwa msangao mkubwa yalipita bila ya umwagaji damu.

kurejesha utulivu na amani nchini ni shida ,kwani uasi wa wafuasi wenye kuvaa fulana nyekundu ukizagaa kama moto nchini kote.Yamkini kuwa wanajeshi na askari polisi wengi wako upande wa waandamanaji hawa wa jazi nyekundu na wafuasi wa waziri mkuu wa zamani Thaksin ambae akiwasaidia watu wa chini na kuboresha hali za wanyonge.

Mwanabiashara huyo na bilionea alichaguliwa kidemokrasi na kwa wingi mkubwa,hatahivyo, sifa hizo hazikumfanya ni mdemokrasi.Ni mwanasiasa anaependa umaarufu tu ambae ameutumia mfumo huo kwa rushua na kujitjirisha zaidi pamoja na kujenga zaidi nguvu na madaraka yake.

Kutoka uhamishoni nje ya nchi, Thaksin anawachochea wafuasi wake kufanya mapinduzi.Nchi Thailand muda mrefu sasa, swali si chama gani kitawale,bali nini mustakbala wa nchi hii na hatima ya ufalme.Jeshi limeapaa kuwa tiifu kwa mfalme na waziri mkuu wa sasa Abhisit Vejjajiva ,kwa asili na jadi yake ni muakilishi wa mabwanyenye wa Bangkok.

Sasa katika barabara za Bangok inaamuliwa iwapo Ufalme ubakie nchini Thailand au baada ya kuaga dunia mfalme ,mzee na mgonjwa Bhumipol Adulyadje ,qasri lake ligeuke jumba la makumbusho.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com