KAMPALA: Uganda kutuma walinda amani Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 23.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA: Uganda kutuma walinda amani Somalia

Uganda imesema leo kuwa iko tayari kutuma wanajeshi 1,500 wa kulinda amani nchini Somalia, kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika, lakini inasubiri kukamilisha taratibu na usafiri wa ndege. Waziri wa ulinzi nchiniUganda, Ruth Nankabirwa, amesema wanaisubiri Algeria ambayo iliahidi usafiri.

Majeshi kutoka Nigeria, Ghana, Burundi na Malawi yanatarajiwa kujiunga na kikosi cha wanajeshi 8000 cha kulinda amani kilichoidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne iliyopita.

Wakati huo huo, serikali ya Uganda imesema waasi 400 wa kundi la Lord´s Resistance Army, wamevuka mpaka na kuingia jamhuri ya Afrika ya Kati, hivyo kuzika matumaini ya kuyafufua mazungumzo ya amani yaliyokwama.

Msemaji wa jeshi la Uganda, meja Felix Kulaije, amesema viongozi wa LRA, Joseph Kony na Vincent Otti walivuka mpaka na wapiganaji wao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com