Kamepni ya kuukomboa mji wa Aleppo na Dresden Magazetini | Magazetini | DW | 18.10.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Kamepni ya kuukomboa mji wa Aleppo na Dresden Magazetini

Mapambano ya kuukomboa mji wa Mossul,jinsi kisa cha kujiuwa gaidi mtuhumiwa Jaber Albakr kinavyolitikisa jimbo la Saxony na Ujerumani kwa jumla,na kuongezeka idadi ya wakaazi nchini Ujerumani magazetini

Tuanzie lakini Irak ambako opereshini kubwa imeanza kuwavunja nguvu wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam-IS au Daesh kama wanavyojulikana. Gazeti la "Nürnberger Zeitung linaandika:

Wakaazi wa nchi za magharibi wanaziangalia kwa hisia za mchanganyiko opereshini kubwa zilizoanzishwa nchini Iraq dhidi ya mji wa Mosul. Kwa upande mmoja watu wanahofia opereshini hizo za kijeshi zisije zikasababisha kwa mara nyengine tena malaki ya watu kuyapa kisogo maskani yao na kutafuta hifadhi katika nchi jirani za ulaya. Na kwa upande wa pili,watu wanatambua vilivyo kwamba IS wanabidi kwanza wavunjwe nguvu ili waweze kurejea nyumbani wakimbizi na kufikiriwa uwezekano wa kuijenga upya nchi hiyo.

 Gazeti la "Südkurier" la mjini Konstanz linachambua suala zima la mapambano dhidi ya IS  likihofia madhara yake kwa wananchi.Gazeti linaandika:"Kuna kinachotokea katika mapambano dhidi ugaidi. Kwa miezi sasa ngome za wanamgambo wa IS nchini  Syria na Iraq zimekuwa zikiporomoka mfano wa barafu katika mchanga wa jangwani. Hivi sasa jeshi la Iraq limeanzisha operesheni muhimu ya kuukomboa mji wa Mossul-ngome muhimu kabisa ya wafuasi hao wa itikadi kali. Pindi mji huo ukikombolewa itamaanisha inatoweka pia ndoto ya kuwepo utawala wa kidini-Khalifa. Hata hivyo pigo lolote katika uwanja wa mapigano IS watalijibu kwa wimbi jipya la mashambulio ya kigaidi barani Ulaya ili kuwatia watu wasi wasi na kuuvunja muungano dhidi yao. Hata kama Mosul utakombolewa mapambano dhidi ya ugaidi bado hayajamalizika."

Kashfa ya kujiuwa Al-Bakr jela mjini Leipzig

Kisa cha kujiuwa jela mjini Leipzig gaidi mtuhumiwa Jaber al-Bakr kinaendelea kugonga vichwa vya habari. Gazeti la "Frei Presse" linaandika:"Serikali ya jimbo la Saxony inazongwa tangu wiki za hivi karibuni na kishindo kikubwa. Makosa chungu nzima yametokea katika kumsaka gaidi mtuhumiwa,raia wa Syria Jaber al-Bakr. Na kisa cha kujiuwa pia baada ya kukamatwa,yote hayo yanazusha masuala ya kuuliza. Majibu kutoka Saxony sio tu ni muhimu kwa jimbo hilo,bali pia kwa serikali kuu na serikali nyengine za majimbo. Kila mmoja anawakodolea macho viongozi wa mjini Dresden. Majibu ya masuala hayo ndio yatakayoamua kuhusu hatima ya sifa iliyoingia madowa ya jimbo hilo la Saxony.

Kizazi chaongezeka Ujereumani

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusiana na kuongezeka idadi ya watoto wanaozaliwa humu nchini. Mitteldeutsche linaandika:"Ni habari za kutia moyo ingawa linasema gazeti hilo la mjini Halle hiyo ni hatua ya mwanzo tu na haiwezi kufunika pengo lilililoachwa na kupungua idadi ya wakaazi humu nchini. Hali hiyo itawezekana ikiwa angalao kila mwanamke mmoja atazaa watoto wawili na ikiwa pia waajiri watarahisisha masharti ya kufanya kazi.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Gakuba Daniel